Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akiwa pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camilius Wambura wakikagua uharibifu uliofanywa na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya St. Anne Marie iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam leo.
Mabasi ya shule na magari mengine yapatayo 17 yamevinjwa vioo na kuharibiwa vibaya.

Maisha ya sasa ni ya sayansi na teknolojia na hii ndio moja ya maabara ya teknolojia hiyo ambayo imeharibiwa vibaya na wanafunzi hao.
DC wa Kinondoni akizungumza na walimu wa shule na viongozi wa shule hiyo.
Walimu wakimsikiliza DC wa Kinondoni
Viongozi wa wanafunzi wakimsikiliza mkuu wa wilaya.