MSANII nyota wa filamu Bongo Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai
kuwa hawezi kuvunja urafiki na meneja wake Martin Kadinda kwa sababu
kama kuna kitu chochote cha mafanikio nyuma yake yupo Kadinda.
Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema.
Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema.
“Kadinda
ndo kila kitu kwangu, hata akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda
mrefu ninapokutana naye tu, nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho
tuliyoachana, hivyo inakuwa kama sijapoteana naye,yaani ni kama vile nipo naye
kila siku iendayo kwa Mungu,”anasema Wema.