Ndugu zangu, naombeni nisieleke vibaya.. Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 26. Nina mwaka wa kwanza tangu nianze kujitegemea mara baada ya kumaliza shule. Nimepanga kwenye nyumba moja iliyoko maeneo ya Mbezi.
Tatizo langu ni kwamba nimetokea kumpenda sana baba mwenye nyumba wangu ambaye ana watoto na familia. Kila nikijibaraguza siwezi. Nimefanya kila mbinu kuzificha hisia zangu lakini nimeshindwa.Kimsingi simpendi mwanamume mwingine zaidi yake.
Tuangaze blog inatoa shukrani kwa wadau wote ambao wanatoa ushauri kwa wadau wengine wanao omba ushauri kupitia blog hii, kiukweli wengi wametoa ushauri na wengi utoa namba zao za simu kwa ajiri ya ushauri zaidi
Basi mpatie ushauri mdau wetu.Bofya hapo chini ili uweze kumpatia ushauri mdau wetu