Hi... Kuna dada yetu anaomba
ushauri wenu. Yeye ni msichana mwenye umri wa miaka 22 ana mchumba na karibuni
wanatarajia kufunga ndoa. Wasiwasi wake ni kwamba anahisi kama yeye sio bikra,
na yeye hajawahi kufanya tendo la ndoa na mwanaume yeyote. Ila ni mara nyingi
anakua anameet na mchumba wake wanafanya kissing, yani kunyonyana midomo,
wanapapasana sehemu zao za siri lakini kila mmoja akiwa amevaa nguo zake
kamili. Wanafanya hayo yote ila hawajawahi kukutana kimwili kufanya tendo la
ndoa. Anauliza jee kufanya hayo yote yanaweza kumfanya kupoteza ubikira wake
bila ya kufanya tendo lenyewe? Na jee ni sababu zipi zinazomfanya msichana
kupoteza ubikira wake? Anaomba ushauri wenu. Shukrani