Wananchi wa Marekani wamechoshwa na vituko, vurugu na uvunjaji wa sheria wa mara kwa mara unaofanywa na star wa Canada Justin Bieber (19), kiasi cha kufikia uamuzi wa kuiomba serikali ya Marekani iingilie kati kwa kupitisha ombi lao la kumrudisha Bieber kwao Canada na kumnyang’anya kibali cha kuishi Marekani.
‘Deport Bieber Petition’ iliyoandikwa kwenda kwa Rais Barack Obama kuomba Bieber arudishwe kwao inasema kuwa, watu wa Marekani wanahisi wanawakilishwa kimakosa katika ulimwengu wa utamaduni wa Pop, hivyo wanaiomba serikali imrudishe kwao Bieber.
Inaendelea kusema sio tu anahatarisha maisha ya vijana wa Marekani lakini pia anawa influence vibaya vijana hao hivyo wanaomba Justin Bieber aondolewe katika jamii yao.
Inaendelea kusema sio tu anahatarisha maisha ya vijana wa Marekani lakini pia anawa influence vibaya vijana hao hivyo wanaomba Justin Bieber aondolewe katika jamii yao.
“We the people of the United States feel that we are being wrongly represented in the world of pop culture. We would like to see the dangerous, reckless, destructive, and drug abusing, Justin Bieber deported and his green card revoked. He is not only threatening the safety of our people but he is also a terrible influence on our nations youth. We the people would like to remove Justin Bieber from our society.”
Hata hivyo Red light inaelekea kuwaka kwa msanii huyo sababu tayari ombi hilo la kufukuzwa kwa Bieber limepata zaidi ya sahihi laki moja ambazo huhitajika ili serikali itoe tamko rasmi juu ya ombi la kufukuzwa kwkae nchini humo. Mpaka saa 2 na nusu usiku wa jana tayari zilikuwa zimepatikana sahihi 100,633.

Bieber haishi nchini Marekani kwa Green Card ambayo humpa mtu ruhusa ya makazi ya kudumu, bali anatumia Visa maalum ambayo hupewa watu maarufu kama waigizaji, wanamuziki, wasomi au watu wengine wenye high profile ambao serikali inaona ni wageni muhimu.
Hata hivyo mashabiki wa dhati wa Bieber wameonekana wakijaribu kumtetea katika website ya Whitehouse, huku wakisema sio haki na hastahili kufukuzwa. “With your help, we can stop it. He’s human. He’s not perfect. The media sees the bad side of him. Please. He’s saved so many lives. Including mine. A lifesaver, Shouldn’t deserve this.” Mmoja wa mashabiki hao aliandika.
Hata hivyo petition hiyo ya kumtetea haikufanikiwa kupata sahihi za kutosha, mpaka Jumatano asubuhi ilikuwa na sahihi 1,400 tu.
Serikali ya Marekani imeahidi kutoa majibu ya petition zinazofikisha sahihi laki moja, japo inaweza kuchukua wiki, mwezi au hata miaka kupata majibu ya serikali juu ya petitions zilizopo ikiwemo ya Bieber.
Source: Washington Times Via Bongo5.com