Mcheza filamu
anayeng’ara katika tasnia ya filamu Bongo Irene Paul ametoa kali ya
mwaka baada ya kudai kuwa hivi karibuni anatarajia kubeba ujauzito na
kujifungua lakini ikifika siku ya kujifungua lazima mumewe awe pembeni
yake akishuhudia akijifungua, hiyo kwake itakuwa ni sehemu ya faraja na
kumuonyesha ni jinsi gani wanawake wanatakiwa kuheshimiwa kwa kuwaletea
watoto wanaume.
Nimepanga nitapoamua kuzaa tu lazima siku ya kujifungua Mr. yaani mumewe
wangu awe pembeni akishuhudia kazi ya kuzaa ilivyo na shuruba maana mtu
mwingine unakuta inafikia muda anakuwa hana mapenzi na mke wala watoto
nina imani akiniona ninavyotabika hatanisumbua wala kukosa mapenzi na
mimi, kama nilivyosema na itakuwa hivyo,”anasema Irene Paul.
Amezidi
kusisitiza kuwa atafanya hivyo katika kujenga mapenzi ya dhati kwa
mumewe kwani shida ambazo upata akinamama wakati wa uzazi wengine hata
uapa kama hawatazaa tena lakini baada ya kujifungua upotea usahau na
kuwa ni jambo la kawaida, Irene anasema anajua wengi watamshangaa lakini
itakuwa kuingilia uhuru wake kwani hata Ulaya wasanii nyota na watu
wengine ujifungua mbele za waume zao labda huku ni kukosekana kwa
ujasiri kati ya wanaume na wanawake pia alimalizia mwanadada huyo.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO