“This is me, mimi ndivyo nilivyo hivi hata kabla ya kuwa Jux mimi nilikuwa hivi,” alisema.
“Kuongea watu wataongea, ukiwa hauko smart watasema labda mchafu, ukiwa smart ‘jamaa bishoo’. Kwahiyo maneno ya binadamu yapo na mimi napokea kila kitu kwangu kwahiyo it’s okay.”
Kuhusu muziki, Jux alidai kuwa kuwa kamwe haufanyi kujifurahisha bali kama kazi japo muda mwingi anakuwa masomoni. “Sifanyi muziki kwa fun sababu natumia muda wangu mwingi sometimes kwenye muziki. Kama sasa hivi nimerudi, natumia muda wangu mwingi sana kufanya muziki. Sometimes silali nafanya nyimbo usiku,” alisema.
“Kitu ambacho watu wengi hawakijui kutoka kwangu mimi, Jux mimi siringi. Kwasababu watu wengi wanajua labda ‘jamaa anajidai, jamaa anaringa’ mimi siko hivyo. Mtu asiyenijua anaweza akanijaji ‘jamaa brother men, ana mapozi anaringa, lakini I am not like that, mimi siringi. Mimi ni mtu poa naongea na kila mtu.”
Jux amewataja Belle 9, Steve R&B na Ben Pol kama wasanii anaowakuli zaidi Tanzania.