
Waumini wa kanisa la ‘World liberation
Ministry’ linalopatikana katika mji wa Sepele nchini Benin walikumbwa na
mshangao baada ya mwanamke mmoja kujifungua farasi wakati wa misa ya
maombi iliyofanyika katika kanisa hilo.
Hata hivyo wakati waandishi wa habari walipofika katika kanisa hilo,
tayari farasi huyo alikuwa ameshakufa. Inasemekana kuwa mwanamke huyo
ambaye jina lake bado halijajulikana, alianza kupiga kelele wakati wa
maombi na kisha kuanza kutoa damu katika sehemu zake za siri kabla ya
kujifungua farasi huyo.
Msimamizi mkuu wa kanisa hilo, muinjilisti Silva Wealth alisema kuwa
bado anashangazwa na kilichomtokea mwanamke huyo. Silva alisema kuwa
wakati wa maombi alipata uono kuwa kuna mwanamke mwenye tatizo na kwamba
kulikuwa kunakitu kinazuia...
Silva aliendelea kusema kuwa maombi yalipopamba kasi, mwanamke huyo
alianza kupiga kelele kisha damu zikaanza kumtoka halafu kikamtoka hicho
kitu.
“Siwezi kuelezea kitu hicho. Katika maombi yetu tumewahi kushuhudia watu
wakitapika vitu mbalimbali, lakini sio kitu kama hiki.” Alisema
muinjilisti Silva.
Mara baada ya taarifa hizo kuzagaa mitaani, watu mbalimbali walianza
kukimbilia katika kanisa hilo ili kuweza kushuhudia kwa macho yao.
Credit-Utamu specially