Muigizaji wa filamu mrembo wa Tanzania, Salma Tamim aka Sabby Angel
ambaye amepata shavu la kuwa chini ya kampuni ya Coastal Films, ya
nchini Kenya, anatarajiwa kuigiza filamu moja na staa wa Nigeria, Ramsey
Noah.
Sabby ameshaonekana kwenye filamu kadhaa za Tanzania ikiwemo ya Hard
Price aliyoigiza na Ray na Nimekubali aliyoigiza na Dr. Cheni, Moto wa
Radi na zingine. Pamoja na kuigiza, Sabby pia ni mwanamuziki.
Mfahamu zaidi kwa picha hizi.