Mcheza filamu
anayeng’ara katika tasnia ya filamu Bongo Irene Paul ametoa kali ya
mwaka baada ya kudai kuwa hivi karibuni anatarajia kubeba ujauzito na
kujifungua lakini ikifika siku ya kujifungua lazima mumewe awe pembeni
yake akishuhudia akijifungua, hiyo kwake itakuwa ni sehemu ya faraja na
kumuonyesha ni jinsi gani wanawake wanatakiwa kuheshimiwa kwa kuwaletea
watoto wanaume.
Nimepanga nitapoamua kuzaa tu lazima siku ya kujifungua Mr. yaani mumewe
wangu awe pembeni akishuhudia kazi ya kuzaa ilivyo na shuruba maana mtu
mwingine unakuta inafikia muda anakuwa hana mapenzi na mke wala watoto
nina imani akiniona ninavyotabika hatanisumbua wala kukosa mapenzi na
mimi, kama nilivyosema na itakuwa hivyo,”anasema Irene Paul.